Exodus 12:43-48

43 a Bwana akamwambia Musa na Haruni, “Haya ndiyo masharti kwa ajili ya Pasaka:

“Mgeni hataruhusiwa kula Pasaka.
44 bMtumwa yeyote ambaye mmemnunua aweza kuila kama mmemtahiri, 45 clakini kibarua yeyote au msafiri haruhusiwi kula.

46 d“Sharti iliwe ndani ya nyumba; msichukue nyama yoyote nje ya nyumba hiyo. Msiuvunje mfupa wowote. 47Jumuiya yote ya Israeli ni lazima waiadhimishe Pasaka hiyo.

48 e“Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya Bwana ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila.
Copyright information for SwhKC